Paroles
Bisimillahi Karima,twakuoomba ya Quddusi,
Mola mwingi wa Rehema,Ilahi mola mkwasi,
Twatoa kauli njema,Twachukuwa hii nafasi,
Salamu zetu twatuma,Zije kwenu kwa wepesi,
(Chorus)
Salamu zetu twatowa,Zende kwa Baba na Mama,
Zipate kuwaongowa,Kwa malezi yao mema,
Daima twaomba duwa,Muzidishiwe neema,
Peponi mwende kutiwa,Pamoja nae hashima,
(Chorus)
Bado twatuma salamu,Ziende kwa kasi sana
Tena hizi ni muhimu Mithili yake hakuna
Zende kwa jombi Adamu,Na mkewe Bi Maimuna
Awahifadhi karimu,In sha Allah tutaonana
(Chorus)
Salamu na mawaridi,Twatuma ziwe faraja
Kwa kaka yetu Saidi,Na mkewe Bi Khadija
Bi Zahara na kaka Sudi,Rabbi awavishe koja
Bi Barika na Muhammadi,Mukidhiwe zenu haja
(Chorus)
Khalidi na dada uba,Pia Abdulrahmani
Wazidishie mahaba,Wahifadhi ya manani
Nuru ya macho na twiba,Luluwa yenye thamani
Abbi kwetu ni dhahaba,Vipenzi vyetu nyoyoni
(Chorus)
Hapa kikomo twakoma,Mangi twataka tuseme
Neno letu la khatima,Ndipo nasi tusimame
Salamu za taadhima,Zende kwa dada fatime
Dada hawaa dada imma,Naomba tusitengane
(Chorus)
Kwa dada yetu fatuma,Tudumu tuelewane
Kwa dada zena twasema,Kwa umoja tushikane
Tusimame wima wima,Kwa pamoja tuungane
Tuwe familia njema,Wala tusibaguane
(Chorus)
Twakuomba maulana,Mikono tumeenuwa
Mola wetu watuona,Hali zetu wazijuwa
Twakuomba ya rabbana,Matozi tunayatowa
Ya illahi subuhana,Takabali zetu duwa
(Chorus)
Ni kwako twategemeya,Sisi ni waja dhaifu
Ilahi twanyenyekeya,Tuna mengi mapungufu
Kwako tunaelekeya,Nyoyo zimejaa khofu
Wapi tutakimbiliya,Kama si kwako latwifu
(Chorus)
Amina rabbi Amina,Tumswalie hashima
Amina rabbi Amina,Rabbi tupe mwisho mwema
Amina rabbi Amina,Rabbi utupe salama
Amina rabbi Amina,Duniani na qiyama
(Chorus)
Style de Musique