AI 노래 생성기 가사 생성기 보컬 리무버 가격 내 노래

Kemea xenophobia

Song generated By ✨Song.do

Song Cover
v1

@ finley nyakundi

2026-09-12 18:39:55

가사

Title: Nyumbani Kwetu Afrika (Sauti ya Kenya)
[Chorus]
Twende, twende nyumbani kwetu Afrika!
Ni kuzuri, ni kuzuri nyumbani kwetu Afrika.
Tukiungana, tukathaminiana, ni kutamu nyumbani kwetu Afrika.
Rangi moja, damu moja nyumbani kwetu Afrika,
Tukemee, tukemee xenophobic syndrome!×2
[Verse 1: Akili na Hekima ya Mkenya]
Kenya si bendera, hatufuati upepo mbaya,
Mwananchi wa kweli ana akili, hekima na busara.
Kando na vivuruge wachache, wezi na wabinafsi,
Mkenya anajua ubaguzi ni ugonjwa wa nafsi.
Mwaafrika kutoka nje si mgeni hapa kwetu,
Yeye ni mwenyeji, ni damu na ndugu yetu.
Hapa ni nyumbani, Kenya iko ndani ya Afrika,
Hatuhitaji kuiga ujinga, chuki isije tukafika!
Twende! Twende! Twende Afrika!
Tanzania—ndugu!
Uganda—ndugu!
Rwanda—ndugu!
Burundi—ndugu!
Congo—ndugu!
Nigeria—ndugu!
Ghana—ndugu!
Ethiopia—ndugu!
Afrika yote—nyumbani!
Hakuna chuki!
Hakuna ubaguzi!
Hakuna xenophobia!
Umoja wetu—nguvu yetu!
Amani yetu—heshima yetu!
Afrika yetu—nyumbani kwetu!
FINAL CHORUS
Twende, twende, nyumbani kwetu Afrika,
Ni pazuri, ni pazuri, nyumbani kwetu Afrika.
Tukiungana, tukathamini,
Ni tamu, ni tamu, nyumbani kwetu Afrika.
Rangi moja, damu moja,
Mipaka haiwezi kututenganisha.
Tukemee, tukemee xenophobia syndrome,
Tukemee chuki, tuishi kwa upendo!×2
[Verse 2: Adui wa Kweli]
Adui mkubwa si ndugu kutoka taifa jirani,
Adui ni ufisadi, ubinafsi, na dhuluma nyumbani!
Ukoloni mambo leo kutoka kwa viongozi wetu,
Ndio unaorudisha nyuma maendeleo ya watu wetu.
Kenya haiungi mkono uongozi mbaya na ukatili,
Tunasimama na utu, upendo ndio yetu ngao na makabilio.
Ukiachilia kando walevi wachache wa chuki na ujinga,
Kenya ni shujaa, ukuta wa amani tunajenga!
[Chorus]
Twende, twende nyumbani kwetu Afrika!
Ni kuzuri, ni kuzuri nyumbani kwetu Afrika.
Tukiungana, tukathaminiana, ni kutamu nyumbani kwetu Afrika.
Rangi moja, damu moja nyumbani kwetu Afrika,
Tukemee, tukemee xenophobia syndrome!×2
[Verse 3: Mipaka ni Mistari, Undugu ni Damu]
Mipaka ni mistari tu iliyochorwa kwa karatasi,
Ila undugu wetu unadumu, hautenganishwi kwa uasi.
Rangi yetu halisi, damu yetu ni moja—Afrika!
Kenya iko kwenye ramani, lakini sote tunashikana.
Mataifa yote kwa pamoja ndio yanaunda bara letu,
Tusiruhusu mambo machache yadhalilishe utu wetu.
Simama kidete, kemea chuki kuanzia leo,
Ili bara letu lisonge mbele kwa heshima na mwangaza mpya!
[Chorus]
Twende, twende nyumbani kwetu Afrika!
Ni kuzuri, ni kuzuri nyumbani kwetu Afrika.
Tukiungana, tukathaminiana, ni kutamu nyumbani kwetu Afrika.
Rangi moja, damu moja nyumbani kwetu Afrika,
Tukemee, tukemee xenophobia syndrome!×2
[Outro]
Afrika simama... Kenya inasema hapana kwa ubaguzi!
Tukumbatie amani, tukumbatie umoja.
Heshima kwa Mwafrika, maendeleo kwa bara letu.
(Twende nyumbani... ni kuzuri Afrika...)
Xenophobia kando! Umoja mbele!
Hapa ni nyumbani kwetu.Afrika!!

음악 스타일

Rhumba sebene Instrumental male voice